
Talaka Si Mke Wangu
Publisher
Ape Network
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
Migogoro katika familia inazua hasira na hasira inazaa talaka. “...Ee chukua... Talaka si mke wangu... Nenda na mimi nipate kutulia roho...” Hivyo ndivyo mume anavyomtaliki mkewe. Mke anaondoka na anashindwa hata kumwaga mwanaye ambaye hata hivyo haifahamiki alipo. Baba analeta mke mwingine na Maisha yanaendelea. Hatma ya malezi ya mtoto iko mikononi mwa Tabia - mke mpya ambaye wala haoni kuwa ana wajibu wa kumlea mtoto wa mwanamke mwingine. “Toto, toto gani hili. Laana tupu”. Talaka ya mama yake inamtelekeza mtoto katika msitu - Ajilee, ajilinde na ajifuatilie mwenyewe! Konaa anapoibuka toka katika msitu huu wa talaka si yeye tena. Ni mtu mwingine ambaye hana nafasi si tu nyumbani kwake bali hata katika jamii yake.