Nyerere na Safari ya Kanaani
Publisher
Ape Network
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on October 26, 2022

TSh 3,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Oktoba, 1966 kulizuka mgogoro mkubwa wa kihistoria kati ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Muhimbili. Wanafunzi hawa walifanya maandamano makubwa hadi Ikulu wakipinga vikali sera ya kuwataka wajiunge na Jeshi la kujenga Taifa (JKT). Wasomi hawa walilalama kwa hasira wakisema, "afadhali wakati wa mkoloni kuliko serekali ya Nyerere. Mkitulazimisha basi tutaenda KIMWILI, lakini MIOYO yetu, aslani, haitaenda JKT..." Katia kuukabili upinzani huu, Mwalimu, katika ile hotuba maarufu: "Tanzania itajengwa na wenye moyo" aliwacharaza viboko baadhi ya wasomi hao kadamnasi na kuwafukuza takribani wanafunzi 400 warudi kwao, wakalime! Mwandishi anatudokeza, miongoni mwa masuala mengine kuwa: Mgogoro huu wa 1966, ulichangia katika kukuza mimba ya safari ya Kanaani nchi asali na maziwa.Hapana shaka kuwa tamthilia hii, iliyoandikwa kwa ustadikabisa, ni kitabu muhimu kwa wanasiasa, wasomi na wapenzi wote wa fasihi ya Kiswahili.