Punje ya Tumaini
Publisher
Lantern - Elizabeth Mramba
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
Fredrick Matata ni kijana mtanashati, wakili na mmiliki wa hoteli kubwa ya kifahari jijini Dar es Salaam. Anajihusisha na starehe za kila aina, wanawake, pombe vyote viliyapamba maisha yake huku watu wakimnyooshea kidole kwamba anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Hata hivyo nani wa kumgusa? Pesa iliongea.
Pasiana msichana mrembo kwelikweli, mwandishi wa habari mwenye kiu kali ya kuokoa vijana dhidi ya dawa za kulevya. Anaingia vitani, shabaha yake ikiwa ni Fredrick Matata. Katikati ya mchezo ghafla karata inabadilika mwindwaji anakuwa mwindaji.