Marimba ya Majaliwa
Publisher
E & D Vision Publishing
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on October 26, 2022

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Je, umeshawahi kusafiri kwa kutumia ungo au fagio? Umeshapanda mgongoni mwa nguva au kutalii kwenye tumbo la nyangumi? Hivi ni baadhi tu ya visa alivyofanya Majaliwa akiwa katika safari yake kuzunguka Tanzania nzima akisaka marimba yake ya nyuzi ishirini. Alianzia Mafia, akaenda Zanzibar, Tanga, Moshi na Arusha, Iringa, Mwanza, Kigoma na miji mingine mingi. Na Kongoti, bingwa wa taifa wa Marimba akimchenga kila mara, huku aking’ang’ania marimba ya Majaliwa ili amzuie kushinda na ashinde yeye. Na bila marimba ya nyuzi ishirini, hakuna ushindi. Je, Majaliwa atamkamata Kongoti? Ungana na Majaliwa katika safari hii ya kusisimua, ukutane na Bibi yake anayeweza kuwa katika umbo lolote, jinsi anavyochenga na kuvisumbua vibwengo huko angani usiku wa manane wakiwa na Majaliwa kwenye ungo. Hutasahau hadithi hii na hutamsahau Majaliwa na safari hii ya kusaka marimba yake. Hadithi ya Marimba ya Majaliwa ilishinda katika shindano la hadihi za kusisimua, mwaka 2007 lililofadhiliwa na Sida na kusimamiwa na Mradi wa Vitabu vya Watoto, Tanzania.