Mwendakizani
Publisher
Active Publisher Ltd
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 04, 2025

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Ule usemi usemwao na baadhi ya watu kwamba karne hii malenga hawapo tena, wamebaki wapanga maneno tu, hata kwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Ushairi umefifishwa kufikia kiwango cha kudorora na si fani yenye hadhi tena, ushairi hauna mvuto mbele ya jamii ya waswahili wenyewe na hata wageni. Usemi huu umejibiwa kwenye diwani hii na kuthibitishwa kwa vitendo kwamba bado malenga wangalipo, tena wenye vipawa vya hadhi ya kuitwa malenga hasa, wenye kukidhi viwango vya utungaji wa mashairi bora aina zote. Ndani ya diwani hii limedhihiridhwa hilo, mshairi hodari mwenye kiwango cha juu, amezima dhana ya kwamba malenga hawapo. Kazi alizozitunga zitawaondolea ukakasi wa mawazo hasi wasemaji hao, ni dhahiri hiki watakachokisoma ndani ya diwani hii kwamba si kile wanachokisema wao, hiki kina hadhi ya karne zile wanazozikubali wao, pasi na shaka yoyote watakiri kwamba wenye kuitambua fani hii bado wangalipo, na wanaiendeleza kwa umakini na uweledi wa hali ya juu. Hii ni karama aliyopewa gwiji huyu, karama ya kuutambua vyema Ushairi wa Kisiwahili misingi na miko yake na kuutendea haki zote, nathubutu kueleza kwamba hakuifanya kazi hii kwa kubahatisha bahatisha. Amefanya kazi iliyotukuka kwa utashi na uweledi wa namna ya pekee.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review

More Books ByActive Publisher Ltd