
Harakati za Ukombozi
Mchapishaji
Ape Network
Lugha
Swahili
MAELEZO YA KITABU
Katika nchi moja ya Afrika, watu wamehangaika kudai uhuru na wameupata. Ila punde wanagundua kuwa wenye dhamana ya kuunda ukombozi wamejiweka mbele katika kufaidi matunda ya ukombozi – wanachota na kufuja rasilimali za nchi kwa manufaa yao peke yao, wanasumbua na kunyanyasa wanyonge na wanakataa miongozo ya haki kwa kujilimbikizia mali. Sasa vijana wana kibarua kigumu cha kutafuta ukombozi wa pili – ukombozi dhidi ya waliokabidhiwa dhamana ya ukombozi. Vijana wanaazimia kuleta mapinduzi ya kweli na kung’oa uhuru wa bendera kwa kuleta uhuru kamili.