BOOK OVERVIEW
Ivana binti mrembo mithili ya malaika, kadhia na shuruba za maisha zinamlazimu kuacha shule kwenda kufanya kazi kama mjakazi katika familia ya kitajiri ya Maxmillian Ayo ili kumsaidia mama yake aliyepooza. Malengo yake ni mawili tu, kutafuta pesa kwaajili ya mama yake baadaye arudi shuleni.
Mambo yanabadilika anapokutana na Easton Maxmillan kijana mtanashati mwenye mvuto wa sumaku.Cheche za huba zinaangaza moyoni mwa Easton mara ya kwanza tu anapomwona bustanini mwa nyumba yao.
Easton yupo mapenzini kwa Ivana hiyo ni simulizi ya kusadikika wanasema anayetaka hachoki, Easton anapambania penzi lake. Penzi jipya linachipua wawili kuwa wanazama dimbwini ndani ya huba zito la siri baina yao.
Kiza kinatanda Easton anapoondoka ghafla kwa safari Marekani, Ivana anapoteza dira. Tafrani ni pale mama Easton anapogundua siri yao, Ivana anatimuliwa ndani ya Jumba la Ayo.
Kiza kinazidi anapobaini kuwa yu mjamzito haki ya mamaye na ugumu wa maisha mambo ni patashika nguo kuchanika. Je nini kitamsibu, Easton atarejea toka ughaibuni? Je ndege hawa wapendanao wataungana tena?