Hidaya ya Penina Muhando Volume Two
Publisher
Ape Network
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 06, 2025

TSh 3,600/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Maandishi ni njia muhimu ya kuhifadhi maarifa, taarifa na utamaduni wa
watu. Kupitia maandishi, simulizi za matukio, hekima na tajiriba za jamii
hunaswa na kufanywa kuishi milele na hivyo kutegua kitendawili cha ukomo
ambao kifo huleta kwenye uendelevu wa mambo. Kupitia maandishi, vizazi
vipya hupata dirisha la kuchungulia kale na kuchota maarifa yanayoweza
kutatua changamoto zao na kuwakinga na mambo yaliyowasibu wahenga.
Bila maandishi, kale hubaki gizani na makosa yanayoweza kuepukika hukosa
kinga ya ufahamu. Bila maandishi, wasia hupotea kama upepo uvumao na
kutowekea nyikani na watunzi hukosa tumaini la ujumbe wao kusikika.
Kwa kuhifadhi masimulizi, jamii hudumisha mapokeo yake, hudhihirisha
utambulisho wake na huenzi urithi wake duniani. Mintarafu ya ufumbuzi
ambao maandishi yamempa mwanadamu, yeye amekuwa ndiye kiumbe
pekee mwenye maisha yenye mwendelezo na matumaini yanayotimizika.
Hata hivyo, maandishi pekee si kitu iwapo hayatatunzwa. Maandishi
yasiyotunzwa ni sawa na hadithi inayosimuliwa kwa hadhira inayosinzia.
Kukosekana kwa maandishi hususan ya fasihi na historia, ni kuiondoa jamii
katika ramani ya ulimwengu ambao kwa kiasi kikubwa unaendeshwa kwa
taarifa na hivyo kuweka mustakabali wa utamaduni wake mashakani.
Kutunza maandishi ni ishara ya uhai, utashi na uwajibikaji wa jamii kwani
huakisi dira na maono ya watu na huenzi mema yaliyokwisha kuvumbuliwa
hivyo, kuepuka kuanza upya au kujikanganya kifalsafa na kimipango.
Mataifa yaliyoendelea yanapowekeza fedha na jitihada za makusudi kutunza
maandishi yake, kusambaza vitabu vyake na kuratibu tafsiri za kazi zao
kwenda lugha nyingine yanafanya hivi kutetea na kuimarisha utambulisho
wao duniani na hivyo kujikinga dhidi ya kumezwa na tamaduni nyingine.
Kwa thamani yake hii kubwa, jukumu la kuhifadhi kazi za maandishi ni
wajibu wa msingi unaohakikisha kuwa jamii ina utambulisho sawasawa na
bendera ilivyo utambulisho wa taifa.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review