
BOOK OVERVIEW
Usiku utakapokwisha ni riwaya inayochambua na kubainisha matatizo yanayoikumba jamii, hususani yale ya kiuchumi, kama vile ukosefu wa ajira. Matatizo haya yanawafanya vijana watatu, Chioko, Gonza na Nelli washindwe kufikia ndoto za maisha yao. Kila wakitamani kupata furaha na tulizo la moyo, shauku yao inagonga mwamba wa dhiki za maisha! Hivyo wanajikuta katika balaa … ndipo tunaposikia kilio cha uchungu cha Gonza akisema, “Kwa nini kabwela tulambe kamasi na wengine asali?” Aidha sauti ya huruma na ushauri ya rafiki yake, Chioko, inasema, “… shida hizi tunazo siku zote. Leo hii hasira
zinakujaje?”
Gonza hakubaliani na hilo. Anaamua kutumia njia ya mkato kushinda dhiki za maisha. Hata hivyo, ndoto na harakati zake zinakatika ghafla ... Yanabaki masikitiko ya Chioko, “Gonza … umemtekenya punda miguu yake ya nyuma, ukapata shukurani zake. Ulitakiwa uwe na subira na utulivu hadi pambazuko ...” Je, nini kilizima harakati za Gonza? Je, usiku utakwisha lini?